Ijumaa , 19th Dec , 2014

Klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam imemtangaza rasmi kocha Hans Van Der Pluijin kuwa kocha mkuu wa Klabu hiyo akirithi mikoba ya Kocha Marcio Maximo akisaidiwa na Kocha Boniface Mkwasa.

Katika Taarifa ya Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga iliyowasilishwa na Ofisa Habari wa Klabu hiyo Jerry Muro amesema mabadiliko hayo yatasaidia kuleta mafanikio katika Klabu hiyo na kufikia malengo waliyojiwekea.

Sanga amewataja viongozi wengine kuwa ni Jonas Tiborowa ambaye atakuwa Katibu Mkuu huku akisaidiwa na wakuu mbalimbali wa idara ambao ni nafasi inayoshikiliwa na Jerry Muro, Omary Kaya akishika nafasi ya Mkuu wa Idara ya Masoko.

Wengine ni Frank Chacha akishika nafasi ya Mkuu wa Kitengo cha Sheria huku Baraka Deusdedit mkuu wa Idara ya Fedha.

Sanga amesema Klabu ya Yanga imeamua kuajiri vijana wengi zaidi katika ngazi za Uongozi ili muda wa kustaafu ukifika Uongozi wa Yanga uweze kubakiwa na warithi Bora.