
Kushoto ni Linex, kulia Domokaya
Domokaya amesema muziki wa sasa hivi ni biashara na watu wamewekeza pesa zao hivyo hawataki kupata hasara ndio maana inatumika njia zote ku-push aina ya miziki hiyo.
"Sasa hivi muziki ni biashara watu wanatia pesa zao, kwa hiyo hawawezi kuweka pesa halafu wakapata hasara hivyo watapush kwa style yoyote hata kama hupendi, zingekuwa zinapata nafasi kazi nzuri na zenye ubora hata kama wasingeweka pesa ingehitajika sapoti tu na mziki mzuri wenyewe utajitangaza" amesema Domokaya
Kupitia comment hiyo aliyoitoa Linex kuhusu kushuka kwa muziki wa Bongo umezua mjadala kwa baadhi ya mashabiki, wasanii na wadau wa muziki mitandaoni.