
Jurgen Klopp
Liverpool wamevuliwa ubingwa wa EPL na Manchester City msimu huu baada ya kikosi hicho kutoka jiji la Merseyside kuutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu uliopita kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 30.
Lakini msimu huu wameshindwa kuutetea ubingwa huo kwa kile kinachoaminika ni kutokana na timu hiyo kukumbwa na majeruhi ya wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza waliokuwa sehemu ya mafanikio ya kikosi hicho msimu uliopita.
"Pamoja na majeraha yetu haukuwa mwaka wa kuwa mabingwa. Kama walivyo wazuri ikiwa Man City wangewakosa mabaeki wao watatu wa kati kwa majeruhi, hapana wasingekuwa mabingwa. Tumepambana kidogo, tumekubali shida na tumefanikiwa, na ikiwa tutashinda Jumapili na tunafuzu Ligi ya Mabingwa basi tutakuwa tumefanikiwa sanaa.” Amesma Klopp
Kocha huyo Mjerumani eneo kubwa la msimu huu alicheza pasipo na uwepo wa mabeki wake watatu wa kati Virgil van Dijk, Joe Gomez na Joel Matip lakini pia kuna wachezaji wengine ambao nao walisumbuliwa sana na majerui msimu huu akiwemo nahodha Jordan Henderson, Fabinho mshambuliaji Diogo Jota ni miongoni mwa wachezaji waliokosekana kwenye michezo mingi msimu huu kutoka na majeruhi.