
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na wajumbe wengine
Kikao hicho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (bara) Ndugu Philip Mangula akisaidiana na Makamu wa Mwenyekiti mwenza (Visiwani) Rais Mstaafu wa Zanzibar Ali Mohamed Shein.
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sehemu ya vikao vya utangulizi kabla ya Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa ambao utafanyika Aprili 30, 2021 jijini Dodoma.