Jumatano , 28th Apr , 2021

Mlinzi wa timu ya kikapu ya Houston Rockets, John Wall na mlinzi wa Orlando Magic, Devin Cannady wamethibitishwa kuwa wataikosa michezo iliyosalia kwenye ligi ya kikapu nchini Marekani NBA msimu huu baada ya wawili hao kupata majeraha makubwa kwenye miguu yao.

Mlinzi wa Orlando Magic, Devin Cannady akiwa kwenye machela na kutolewa nje baada ya kuvunjika kifundo cha mguu.

Wall aliyepata maumivu ya misuli kwenye mchezo dhidi ya Los Angeles Clippers Aprili 23, 2021, usiku wa kuamkia leo amefanyiwa vipimo vya MRI na kuonekana kuathiriwa pakubwa kwenye misuli yake ya paja hivyo ataikosa michezo ya timu yake iliyosalia NBA msimu huu.

Wall ambaye msimu mpya na Rockets umeingia dosari licha ya kuonesha kiwango safi, amefanikiwa kucheza michezo 40 pekee akiwa na wastani wa kuipatia timu yake alama 20.6, rebaundi 3.2, assisti 6.9, kupora mipira asilimia 1.1 na asilimia 40 za kupiga mashuti.

Kukosekana kwa John Wall kunazidi kuipata wakati ngumu Houston Rockets kwani tayari wana rekodi mbaya ya kufungwa michezo 46 na kushinda 15 pekee kwenye NBA msimu huu ikiwa ndiyo timu iliyopoteza michezo mingi zaidi.

Kwa upande mwingine,

(Mlinzi wa Washington Wizard, John Wall)

Devin Cannady nae atakosa michezo yote iliyosalia msimu huu kwenye NBA baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye kifundo chake cha mguu kilichovunjika usiku wa kuamkia siku ya Jumapili wakati timu yake ya Orlando Magic ilipokuwa ikicheza na Indiana Pacers.

Nae kocha msaidizi wa Devin, Tyrone Corbin amesema “Anatarajiwa kupona ba hiyo taarifa nzuri kwake”. Tyrone ameyasema hayo baada ya kupewa taarifa hizo na daktari mkuu aliyesimamia upasuaji wa nyoyta huyo.