
Rais wa FIFA, Gianni Infantino.
Kwa niaba ya wajumbe wa jumuiya ya soka kimataifa, Rais wa jumuiya hiyo Gianni Infatino ameandika kuwa:
“Ilikuwa hisia ya huzuni kupata taarifa za kifo cha Rais Dk.John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.”
“Tunapenda kuungana na wote wanaotoa salam za pole kutoka pande zote Duniani.”
“Akiongoza toka mwaka 2015, kiongozi mwenye haiba ya juu, aliyetambulika kwa maono yake, uzalendo, matendo ya Utawala bora na kupiga vita rushwa na umasikini, Rais, Dk.John Pombe Magufuli hatosahaulika”.
“Kwa niaba ya wajumbe wa jumuiya ya soka kimataifa, tunapenda kutoa pole kwa shrikisho la soka nchini Tanzania 'TFF', serikali na watanzania kwenye kipindi hiki kigumu”.