Ijumaa , 14th Nov , 2014

Timu ya Taifa,Taifa Stars imewasili leo Mbabane nchini Swatsland ikitokea nchini South Africa kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya timu ya Taifa ya Swatsland ya kalenda ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA inayotarajiwa kuchezwa Jumapili.

Akizungumza jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Soka nchini TFF,Boniface Wambura amesema kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mart Nooij kimepokelewa na Ofisa Mtendaji mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini Swatsland.

Wambura amesema mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa saa tisa na nusu kwa saa za Swatsland huku kwa hapa nchini ikiwa ni saa kumi na nusu.