Alhamisi , 10th Dec , 2020

Katika kufikia kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC) imesema sheria imeweka utaratibu kwa wanandoa kuweza kutalakiana ili kuepusha ukatili wa kijinsia unaoweza kujitokeza kutokana na mizozo baina yao.

Akizungumza katika kipindi cha SupaBreakfast mwanasheria kutoka LHRC, Victoria Lugendo, amesema jamii inapaswa kujua kuwa haki za binadamu kila mmoja amezaliwa nayo

“Maendeleo yanahitaji uwekezaji na maendeleo yanaendana na haki za binadamu, katika kuadhimisha kilele cha ukatili wa kijinsia , sheria imeweka utaratibu kama ndoa imefika hatua huwezi kuendelea sheria hipo chukua talaka ili kuepusha vitendo vya ukatili” amesema Victoria

Aidha Victoria amesema kuwa haki za binadamu nchini zinalindwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano huku akieleza hatua mbili zakuchukua endapo haki yako imevunjwa; “Zipo aina mbili mbili zakuchukua hatua kama haki yako imevunjwa kuna usawa na wima, serikali si serikali inavunja kwenye usawa ni mimi na wewe, na wima unapanada juu hatua inachukuliwa ambapo mtu aliyevunja ni serikali"