Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia na kulia ni Mbunge mteule wa jimbo la Vunjo Dkt. Charles Kimei.
Dkt Kimei amempiga chini Grace Kiwelu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye amepata kura 8,675, na kufuatiwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo James Mbatia aliyepata kura 4,949 na Agustino Mrema wa chama cha TLP kwa kupata kura 606.
Dkt Kimei anaongoza jimbo hilo ambalo hapo awali kabla ya Bunge la 11 kuvunjwa, lilikuwa likiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia.