Ijumaa , 23rd Oct , 2020

Bodi ya ligi Tanzania bara TPLB imetangaza kufungwa kwa viwanja viwili kwa mechi za ligi kuu ambavyo ni Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na Jamhuri jijini Dodoma mpaka taarifa nyingine itakavyotolewa.

Simba na Yanga zimekuwa zinautumia uwanja wa Mkapa kwa mechi zao za nyumbani na sasa vitatumia Uwanja wa Uhuru

Taarifa iliyotolewa na TPLB ni kwamba mechi zote za ligi kuu msimu huu wa 2020/21 zilizopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam zitachezwa uwanja wa Uhuru hadi hapo uwanja huo utakapofunguliwa.

Wakati huo huo mechi zote za ligi kuu zilizokuwa zichezwa uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma sasa zitachezwa katika uwanja wa Samora mjini Iringa na zile za ligi daraja la kwanza zitachezwa uwanja wa Jamhuri Morogoro .

Klabu kongwe hapa nchini Simba na Yanga zimekuwa zinautumia uwanja wa Mkapa kwa mechi zao za nyumbani na sasa vitatumia Uwanja wa Uhuru.

Hapo jana klabu ya Yanga iliutumia uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wake wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania mchezo amba walishinda goli 1-0 wakati Simba watautumia uwanja huo katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting Oktoba 26 mwaka huu.

kwa mujibu wa taarifa uwanja wa Jamhuri Dodoma umefungwa kupisha marekebisho kwa ajiri ya shughuli maalum za Chama cha mapinduzi na Serikali zitakazo fanyika wiki ijayo.

Kwa Uwanja wa Jamuri umekuwa ukitumiwa na timu timu za JKT Tanzania pamoja na Dodoma jiji FC.