Jumanne , 20th Oct , 2020

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ambaye pia ni  mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Tanga Mjini, leo tarehe, 20, Oktoba akiwa katika kampeni za mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM huko Korogwe (Tanga) amesema kuwa Dkt. John Magufuli amepunguza misiba mingi.

Waziri wa Afya ambaye pia ni mgombea wa Ubunge, Jimbo la Tanga Mjini kwa tiketi ya CCM

Waziri Ummy amebainisha hayo huku akiyataja maboresho makubwa yaliyofanywa katika sekta ya afya kuwa chachu ya kupunguza misiba katika familia za Watanzania ambapo amegusia suala la kupungua kwa vifo vya akina mama na watoto huku akitaja maboresho ya vituo vya afya na miundombinu ya matibabu na vifaa tiba kuwa imeimarika maradufu.

"Magufuli amepunguza misiba katika familia za Kitanzania, amepunguza misiba ya akina Mama wajawazito,  vifo vimepungua kutoka Elfu 11 kwa mwaka vya wajawazito hadi vifo Elfu 3 kwa mwaka, haijapata kutokea dunia nzima"  Ummy Mwalimu.

Aidha Ummy ameongeza kuwa " Vifo vya watoto wachanga katika vizazi hai vimepungua kutoka 25 hadi 7 kati ya vizazi  elfu 1000 pia vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano vimepungua kutoka 67 hadi 11 katika kila vizazi hai elfu 1000.