Jumanne , 13th Oct , 2020

Mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, ameahidi kuimarisha biashara katika mkoa wa Tanga, kufufua viwanda vilivyokufa pamoja kutoza kodi rafiki kwa wafanyabiashara ili kuinua uchumi wa nchi.

Mgombea urais kupitia CUF Profesa Ibtahim Lipumba, akizungumza na wananchi wa mkoa wa Tanga

Akiongea katika mkutano wa hadhara wa kampeni mkoani Tanga Prof. Lipumba amesema kwamba huwezi kuwa na uchumi mzuri bila ya kuwa na mfumo mzuri wa fedha pamoja na ongezeko la ujazo wa fedha ndani ya nchi.

“Hali ya upatikanaji wa fedha kwa sasa ni ngumu, wananchi wanahali ngumu na baadhi ya biashara zinafungwa, sisi CUF mkitupatia ridhaa tutafufua viwanda, tutaweka mfumo mzuri wa fedha na kuongeza ujazo wa fedha", alisema Prof. Lipumba.

Akizungumzia madai ya kuwepo kwa vitisho kwa viongozi wa CUF Tanga, Prof. Lipumba amesema kwamba CUF inataka kuwapo kwa siasa za amani na wala si za vitisho kwa kuwa chama hicho kinaamini katika haki sawa kwa wote.