
Mgombea urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu.
Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 2, 2020 na Katibu wa kamati ya maadili ya kitaifa Emmanuel Kawishe, ambapo imedaiwa kuwa maneno hayo ya uchochezi aliyatoa akiwa mkoani Mara na Geita na kamati imeridhia kuwa Lissu amekiuka maadili ya uchaguzi.
Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa barua ya kumtaka Lissu kujibu tuhuma hizo iliwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, ambapo alijibu kuwa malalamiko hayakihusu chama, na hivyo kamati hiyo imeridhia kuwa taarifa kuhusu malalamiko ya ukiukwaji wa maadili iliwasilishwa kwa mlalamikiwa kwa kuwa CHADEMA ndiyo ilimdhamini kuwa mgombea wa urais, hivyo barua kuwasilishwa kwa katibu mkuu ni sahihi kabisa.