
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Karume kata ya Ilala, Haji Bechina,
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Karume kata ya Ilala, Haji Bechina, amesema vijana hao wamekuwa kero si kwa wananchi wanaofika sokoni hapo bali pia hata kwa uongozi wa soko.
“Tumekuwa tukipokea malalamiko mengi sana kuhusu hawa vijana hivyo kwa sasa tumeanza kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwaondoa kabisa” amesema Bechina
Amesema vijana hao wamekuwa wakichafua taswira ya soko kutokana na vitendo wanavyovifanya ikiwa ni pamoja na uhalifu lakini pia na kuwabugudhi wateja ambao wanafika katika soko hilo kwa ajili ya mahitaji mengine