
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Mama Samia Suluhu.
Akizungumza hii leo Septemba 27,2020 katika muendelezo wa kampeni zake zilizofanyika katika wilaya ya Kongwa amesema kuwa serikali inafahamu kwamba mkoa huo unakabiliwa na uhaba wa maji ambapo pia ameahidi kuendeleza utoaji wa Elimu bila malipo.
''Tunajua kuna shida ya maji na tuakuja kuleta maji, tunajua changamoto za uhaba wa maji ziko maeneo mengi ndani ya Dodoma, lakini ndani ya Mpwapwa lakini serikali ndani ya miaka mitano ijayo inakuja kutekeleza miradi mikubwa ya maji'' amesema Samia Suluhu.
''Tunakwenda kuendelea na lile la kusomesha watoto wetu wa kitanzania elimu bila malipo,mzigo huu umebebwa na serikali kutoka kwa wazazi,sasa wengine waje waseme hapa wanakuja kuleta elimu ya aina gani''ameongeza
Aidha amesema kuwa kuna mengi yanayofanyika na yatakayoendelea kufanyika ikiwemo kufufua Shirika la Ndege kuongeza bandari nchi nzima,kujenga meli na vivuko,pamoja na kufufua reli za zamani.