Alhamisi , 30th Oct , 2014

Vilabu vya mchezo wa mpira wa mikono kutoka nchini Kenya vinatarajia kushiriki michuano ya Mpira wa mikono ya Kemoma Cup inayotarajiwa kutimua vumbi Novemba 24 mpaka 29 Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Mikono nchini TAHA, Nicholaus Mihayo amesema wamealika vilabu mbalimbali kutoka Kenya, Uganda, Zanzibar na wenyeji Tanzania Bara ambapo Kenya wameahidi kuleta timu mbili, Zanzibar pia imeahidi ushiriki huo huku Tanzania ambao ni wenyeji wakihakiki ushiriki wa michuano hiyo.

Mihayo amesema vilabu kutoka nchi ya Uganda ambapo bado hawajahakiki ushiriki huo, walishafanya nao mawasiliano na wanategemea kupokea uhakiki wa ushiriki wa michuano hiyo mwanzoni mwa mwezi Novemba.