
Rais wa Barcelona Joseph Maria Bartomeu akihutubia katika moja ya mikutano ya klabu
Lionel Messi aliwasilisha maombi rasmi kwa Uongozi wa Timu ya Barcelona akitaka kuondoka katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi, suala lililoleta taharuki kubwa kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo duniani kote.
Bartomeu anatuhumiwa kuzembea hadi Messi kuchukua hatua hii, japo ukweli ni kuwa kichapo cha bao 8-2 dhidi ya Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali ya Mabingwa Barani Ulaya ndio iliyo sababisha haya yote huku kocha Quique Setien na Mkurugenzi wa ufundi Eric Abidal wakifukuzwa kazi.
Barcelona walipanga kufanya uchanguzi wao wa kawaida kwa mujibu wa katiba yao mwaka 2021 ambapo Raisi huongoza kwa kipindi cha miaka minne, huku washindani wengine katika nafasi hiyo wakitumia sakata la Messi kama sera wakati wa uchanguzi.