Jumatatu , 3rd Aug , 2020

Kamati ya Nidhamu ya TFF imemfungia Kocha Luc Eymael miaka miwili na kumtoza faini ya jumla ya Tsh. Milioni 8 kwa kosa la uchochezi na ubaguzi.

Kocha wa zamani wa Yanga Luc Eymael

Mjumbe wa kamati ya Nidhamu ya TFF, Alex Mushumbuzi amesema wameridhika na ushahidi uliotolewa dhidi ya kocha huyo na ataanza kutumikia adhabu hiyo kuanzia leo.

Hata hivyo, Mushimbuzi amesema Kocha huyo ambaye tayari amefukuzwa kazi na Yanga ana haki ya kukata rufaa katika ngazi ya juu ambayo ni Kamati ya Rufaa ya TFF (Shirikisho la Soka Nchini).

Eymael anatuhumiwa kufanya kosa hilo baada ya mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli ambapo Yanga ilishinda bao 1-0, mechi iliyochezwa Uwanja wa Samora Mkoani Iringa.