Jumatano , 17th Jun , 2020

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenda Nchini Burundi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Burundi Mhe Evariste Ndayishimiye kesho, June 18, 2020.

Rais Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema hayo Jijini dar es Salaam katika Ubalozi wa Burundi Nchini Tanzania alipokwenda kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza aliyefariki Juni 09, 2020 kwa maradhi ya moyo.
 
Ameongeza kuwa kutokana na mahusiano ya karibu yaliyopo baina ya Burundi na Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameamua kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenda Burundi ambapo mbali na kuongozwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan pia ataambatana na Rais Mstaafu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.