Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania
Wakizungumza na EastAfrica Radio baadhi ya wananchi hao wamesema Mwl Nyerere alikuwa tayari katika kupambana na kuwashinda maadui umaskini, maradhi na ujinga kwa kuboresha mfumo wa elimu nchini ikiwemo jitihada za kukubali kuyazika maslahi yake binafsi kwa ajili ya wengi.
Aidha wamesema kuwa suala la uoga ndio limekuwa adui mkubwa wa maendeleo ya elimu na Taifa kwa ujumla na limezuia mabadiliko chanya ambayo yangeweza kutokea ili kulikomboa taifa ikiwemo upatikanaji wa elimu bora ambayo inamjenga mwanafunzi kujitegemea.
Wakati maadhimisho haya ya kitaifa yatafanyika mkoani Tabora, yakiambatana na kuzimwa kwa mwenge wa uhuru, familia ya Mwalimu, muasisi wa Taifa la Tanzania wao wameadhimisha misa ya kumuombea mwalimu anayetajwa kuwa mwenye heri na harakati za kumtangaza zikiendelea, familia hiyo imesalia kijijini Mwitongo, na kudai kuwa siku hadi siku kumbukizi hiyo inapoteza maana.