Jumanne , 14th Apr , 2020

Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia CHADEMA Wilfred Lwakatare, leo Aprili 14, 2020, amesema kuwa kwa sasa atapumzika katika siasa ambazo amezitumikia kwa miaka mingi na kwamba hana deni na mtu yeyote hata wale ambao aliwahi kuwashinda alishamaliza nao.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, na Mbunge wa Bukoba Mjini Wilfred Lwakatare.

Hayo ameyabainisha Bungeni Dodoma, wakati wa Mkutano wa 19, kikao cha saba cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Leo nashukuru Mungu kwamba nafuata nyayo za Mama Tibaijuka na Mheshimiwa Bulembo kwamba napumzika katika siasa ambazo nimezitumikia kwa miaka mingi, sina deni wala kitu chochote waliowahi kunishinda nimemaliza Bunge nikiwa nimewashinda" amesema Mbunge Lwakatare.