Mkali wa BongoFleva Alikiba
Sasa muda mfupi uliopita Alikiba ameweka maelezo katika mtandao wa Instagram, ambayo inatafsirika kama fumbo flani hivi baada ya wasanii wake kujitoa katika lebo ambayo yeye anaisimamia.
Katika post hiyo Alikiba ameweka picha ya mkongwe wa BongoFleva Dully Sykes kisha ameandika "Unapomtendea mtu jambo lake tena kwa mapenzi yote usitarajie fadhila wala malipo baadae kwa sababu kuna aina nyingi ya binadamu, sio kila mmoja ana moyo kama wako".