Msanii wa singeli Dulla Makabila
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Dulla Makabila amesema binafsi hapendi wanawake wasio na vipato kwa sababu yeye mwenyewe bado anatafuta pesa.
"Mimi sio mtu wa dizaini ya marioo au king'asti, natafuta pesa zangu mwenyewe, ila ni mtu ambaye nina bahati ya kupendwa na wanawake ambao wapo vizuri kimaisha na wenye pesa sio kwamba ndiyo ninaowatafuta, kwa sababu sisi wanaume kuigiza hatujui kama unampenda mwanamke kwa ajili ya pesa zake atajua tu" Dulla Makabila.
Aidha msanii huyo ameongeza kwa kusema "Pia ninampenda mwanamke mwenye kipato na hata asingekuwa na kipato bado ningempenda tu".