Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
Mhandisi Masauni ametoa kauli hiyo wakati akiongea na wakimbizi kutoka nchini Burundi, walioko katika Kambi ya Nduta wilayani Kibondo mkoani Kigoma, huku akiwataka wakimbizi hao kuendelea kujiandikisha kurudi nchini kwao ambako amani imerejea.
"Serikali ya Tanzania inawapenda sana ndugu zao wa Burundi, lakini si nchi ya kubembeleza watu waovu, baadhi ya watu wamekuwa wakiingia kambini na wanatoka na kwenda kufanya uhalifu nje, kuna watu zaidi ya 1000 walitoroka na hao tayari wameshajivua kuwa wao ni wakimbizi, hao ni wahamiaji haramu na ninashangaa kwanini hadi sasa hivi wapo" amesema Naibu Waziri Masauni.



