Wachezaji mbalimbali akiwemo Samatta, Ronaldo, Messi na Ramos
Barani Ulaya mechi kubwa katika Ligi Kuu ya Hispania La Liga ni kati ya vigogo wawili Real Madrid watakaokuwa wenyeji wa Barcelona.
Mchezo huo utakaopigwa Jumapili Saa 5:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, mpaka sasa haujawekwa wazi kama kutakuwa na tahadhari yoyote kwa mashabiki juu ya virusi vya Corona.
Barcelona wanaongoza ligi wakiwa na pointi 55, Real Madrid wakiwa na pointi 53 katika nafasi ya pili.
Kwa upande wa Ligi kuu ya Italia mechi kali inatarajiwa kuwa kati ya vinara Juventus wenye pointi 60 dhidi ya Inter Milan waliopo nafasi ya 3 wakiwa na pointi 54.
Hata hivyo mashabiki hawataingia uwanjani kutoka na tishio la virusi vya Corona.
#FAHAMU Serie A na mamlaka za afya nchini Italia zimefikia uamuzi wa kutoruhusu mashabiki kuingia uwanjani katika mechi za ligi kuu wikiendi hii, ikiwemo zile ya Jumapili Juventus Vs Inter Milan, AC Milan Vs Genoa, hii ni kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya Corona. pic.twitter.com/JvKeRNRVTS
— East Africa TV (@eastafricatv) February 28, 2020
Nchini England kwenye ratiba ya ligi kuu, ulipangwa kuchezwa mchezo wa Premier League kati ya Man City dhidi ya Arsenal lakini fainali ya kombe la Carabao ikasababisha mabadiliko na sasa mchezo utakaopigwa jumapili ni kati ya Man City dhidi ya Aston Villa anayochezea Mbwana Samatta.
Fainali hiyo itapigwa Saa 1:30 kwa saa za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Wembley.
Mpaka sasa hakuna zuio lolote kwa mashabiki kuhudhuria mchezo huo wa fainali ya kwanza kwa Nahodha Mbwana Samatta.

