Ijumaa , 3rd Oct , 2014

Mashindano makubwa kabisa ya kudansi ya Dance 100 2014, yameanza leo baada ya kila kitu kukaa katika mstari tayari kwa mpambano mkali wa makundi 5 kuwania taji kubwa la ukali wa dance Afrika Mashariki kwa mwaka huu.

mashindano ya kudansi nchini Tanzania ya Dance 100 2014

Mbali na mchuano mkali kutoka kwa makundi haya matano, fainali za mashindano haya yaliyoanza kwa kasi leo katika ukumbi wa Don Bosco Oysterbay, yameandaliwa na burudani kali ya muziki kutoka kwa wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa katika tasnia ya muziki.

Katika swala zima la zawadi kwa washindi, ili kuiongeza motisha Juu ya shilingi milioni 5, kundi litakaloshinda hii leo litapatiwa simu kutoka vodacom pamoja na muda wa maongezi kwa kila dansa, na mbali na zawadi kutoka Grand Malt, Mshindi pia atakabidhiwa Kombe.

Swali lenye kilo zisizohesabika likibaki kuwa ni kundi gani litakalochomoka na ushindi kati ya The WT, Wakali sisi, Best Boys, Wazawa Crew na The winners Crew.