RPC Manyara, Paul Kasabago.
Akizungumza leo Januari 10, 2020, Kamanda wa Polisi mkoani humo Paul Kasabago, amesema kuwa mtuhumiwa huyo aliwachukua watoto hao, wakiwa njiani kuelekea shuleni majira ya saa 5:00 asubuhi.
"Mtuhumiwa huyo aliwalaghai kwa kuwapa Shilingi 500 ndiyo akawa amewavutia makaburini yaliyokaribu na shule hiyo na kuwalawiti kwa zamu, huku akiwatishia kwamba atawaua endapo hatokiri matakwa yake, watoto walitibiwa na kuruhusiwa na tunaendelea kumtafuta huyo mtuhuniwa" amesema Kamanda Kasabago.
Katika hatua nyingine Michael Donati (25), amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la ubakaji wa mwanafunzi wa Darasa la Sita.
	 

