Jumatatu , 29th Sep , 2014

Bendi ya muziki ya Malaika, imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na moja ya wanamuziki wake anayefahamika kwa jina Adaya, ambaye amepoteza maisha siku ya jana jijini Dar es Salaam baada ya kuugua malaria.

aliyekuwa mwimbaji wa bendi ya Malaika nchini Tanzania marehemu Adaya

Akiongea na eNewz kuhusiana na tukio hili, Kiongozi wa Bendi ya Malaika, ambaye amerejea Dar akitokea Morogoro leo Christian Bella, amesema kuwa anasikitika kwa msiba huu na siku ya leo wanatarajia kukutana kwa ajili ya kuweka mipango ya msiba, na hapa anaeleza.