Alhamisi , 2nd Jan , 2020

Msanii wa muziki nchini AT, amesema kuwa hana mpango wa kufanya kazi ya kimuziki na wasanii wa Afrika kwa sababu haoni utofauti wowote kutoka kwao na badala yake anafikiria kufanya muziki na msanii wa Pop kutoka nchini Marekani, Justin Bieber.

Msanii wa Bongo AT na Msanii wa Pop nchini Marekani Justin Bieber.

AT ameyabinisha hayo leo Januari 2, 2020, kwenye kipindi cha DADAZ kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana na kusema kuwa anataka kufanya muziki ambao utaleta utofauti mkubwa.

"Sitaki kufanya kazi ya muziki na waafrika, mimi napenda kufanya kazi na Justin Bieber" amesema AT.

Aidha msanii huyo ameongeza kuwa wasanii wengi wa Tanzania, wanaangalia soko la ndani pekee na kwamba hakuna msanii ambaye ataweza kuimba wimbo ambao utakuwa na ladha sawa kama wimbo wake wa Nipigie.

"Wasanii wengi wanaangalia market ya ndani tu ndio maana wasanii wakubwa nchini hawapandi Ndege wanaishia kupanda mabasi tu, ndio maana hadi leo huwezi kusikia muziki kama Nipigie, watu sasa wanaimba muziki unafanana tu kama Wajapan" amesema AT.