
Picha za baadhi ya wasanii waliofanya matukio 2019.
VIFO
Kwenye sekta ya burudani ilishuhudiwa tukio la simanzi na majonzi, baada ya taarifa zilizotoka siku ya Februari 13 juu ya kufariki kwa Godzilla, ambaye alikuwa anasumbuliwa na homa kali pamoja na tumbo, vifo vingine vilivyotokea ni msanii wa kundi la The Mafik aitwaye Mbalamwezi, Msanii wa filamu Mama Abdul na Bibi Cheka.
KIKI
Moja kati ya kiki iliyotokea kwa mwaka 2019 ni juu ya msanii Harmorapa kuwa kwenye mahusiano na mzungu, ambaye anadai alikuwa ni dada wa JayZ, kiki nyingine aliyoitoa msanii huyo ni kuongea lafuzi ya Kenya.
MAHUSIANO
Mwaka 2019 kwenye suala la mahusiano yalitaradadi sana, kuanzia wasanii waliopata mahusiano mapya na yaliyovunjika. Mahusiano mapya tuliyoyashudia ni penzi la Tunda na Whozu, Yusuph Mlela na Ebitoke, Jux na Nnayika,Vanessa Mdee na Rotimi.
Moja kati ya habari kubwa katika penzi lililovunjika ilikuwa kati ya Jux na Vanessa Mdee, kwa sababu wasanii hao walipokuwa wapenzi walishawishi na kuvutia watu wengi kwa kuwa walikuwa wanafuatiliwa sana na watu.
Kuvunjika kwa ndoa ya Chidi Mapenzi na Shamsa Ford, ilikuwa moja ya taarifa iliyozua gumzo mwaka 2019.
Mwisho ni kuvunjika kwa mahusiano ya Ebitoke na Yusuph Mlela, ambapo tulishuhudia ugomvi kutokea siku ya Novemba 11, baada ya Ebitoke kuvamia mkutano wa Yusuph Mlela na waandishi wa habari hali iliyopelekea kupigana na mpenzi mpya wa Yusuph Mlela.
KUTOKA MITANDAONI
Moja kati ya vitu vilivyotrend kutoka katika mitandao ya kijamii nikusambaa kwa picha na video zilizokosa maadili, zikimuonesha msanii wa filamu Menina ambaye nusu ya maungo yake yakiwa wazi, hali iliyopelekea kuitwa na Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA ) ili kuchunguza juu ya tukio hilo.
Vitu vingine vilivyotrend kutoka katika mitandao ya kijamii ni aina ya misemo na maneno ambayo yamezungumziwa sana na watu, wasanii na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Neno Connection, Baharia, Mwanaume na nusu, Mwanaume wa Kinondoni, Watu wa Buza, na Kujimwambafai yametumika sana kwenye mitandao ya Instagram,Twitter, Whatsapp na Facebook.