
Vanessa Mdee na mpenzi wake Rotimi walipotua Bongo
Kupitia Insta stori zao za kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram, wawili hao wameonesha picha na kuwa tayari wamekwishawasili hapa nchini na zingine wakiwa kwenye gari.
Wawili hao wanatarajia kufanya show ya kufunga mwaka na kufungua mwaka mpya, siku ya leo ya Disemba 31, 2019, katika moja ya sehemu ya starehe iliyopo Kawe Beach Jijini Dar Es Salaam.
Ikumbukwe tu wawili hao wameanza mahusiano yao ya kimapenzi mwezi Oktoba 2019 na habari yao ya kuwa kwenye mahusiano iliripotiwa na vyombo vingi vya habari kwenye upande wa burudani.