Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera John Joseph.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Oktoba 30, 2019, Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera John Joseph, amesema kuwa Septemba 23 mwaka huu walipata taarifa ya Wambura kujihusisha na vitendo vya kuomba rushwa.
Aliomba rushwa kutoka kwa baadhi ya wafugaji wenye uhitaji wa vitalu vya kufugia ng’ombe, au wenye vitalu ambao wanahitaji kuhuisha mikataba yao ya awali.
Aidha mkuu huyo wa TAKUKURU amesema kuwa wamewafikisha mahakamani watu wengine wanne ambao wanakabiliwa na mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa.



