Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanale akiwa na wengine katika shule ya Sekondari ya Sokoine Memorial.
Mkuu huyo wa mkoa amebaini hilo katika ziara yake, iliyolenga kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani Mvomero, ambapo akiwa katika mradi wa shule hiyo ameshangazwa na mradi huo kutumia fedha nyingi, lakini ni miaka saba sasa imepita bila mradi huo kukamilika.
Aidha ameagiza serikali ya wilaya hiyo kuhakakikisha wanamalizia sehemu iliyobaki ili shule hiyo ianze kupokea wanafunzi katika muhula wa masomo wa mwaka 2020.
Akiwa katika mradi wa hospitali ya wilaya ya mvomeoro mkuu wa mkoa anaridhishwa na hatua iliyofikiwa ambapo Mkurugenzi wa halmashauri ya hiyo, Frolent Kayombo ambaye amesema mradi huo umetumia kiasi cha milioni mia tano hamsinia na tatu ambapo huduma zote zitaanza kutolewa ndani ya wiki mbili zijazo ikiwemo huduma ya uzazi kwa wakina mama wajawazito.

