Jumatano , 25th Sep , 2019

Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu Dar es salaam, imekataa maombi ya viongozi wawili wa CHADEMA, Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Vincent Mashinji, pamoja na Mbunge wa Tarmime Mjini, Ester Matiko.

Upande wa utetezi uliwasilisha maomboi hayo jana Septemba 24, 2019 ambapo walipendekeza Mahakama kutoa ruhusa ya viongozi usafiri nje ya nchi, ambapo Hakimu Simba amesema kama akiwaruhusu watuhumiwa hao kusafiri kesi itachukuwa muda kuisha.

"Nikiwaruhusu kusafiri na wengine wakiomba kusafiri sitaweza kuwakatalia na matokeo yake kesi itachukua muda kuisha" amesema Hakimu Thomas Simba

Kesi hiyo ya uchochezi inawakabili viongozi tisa wa CHADEMA, hadema, imehairishwa hadi oktoba 7/2019 itakaposikilizwa kwa siku tano mfululizo kuanzia tarehe 7 hadi 11 mwezi oktoba, viongozi wengine waliopo kwenye kesi hiyo ni pamoja na Mchungaji Peter Msigwa, John Heche, Halima Mdee, Ester Bulaya, John Mnyika, na Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar Salum Mwalimu.