Jumanne , 24th Sep , 2019

Baadhi ya wanaume katika Kijiji cha Fulwe, mkoani Morogoro wanaachiwa watoto na wake zao kwa ajili ya kuwatunza hasa inapofika nyakati za usiku, kutokana na wake zao kulazimika kuamka nyakati hizo na kwenda kutafuta maji, kwa ajili ya matumizi ya majumbani.

Wakizungumzia hali hiyo, baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho wamesema wanaamka usiku wa manane ili kusubiria maji kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo kwa muda mrefu na kupelekea wanaume kuachiwa watoto kila inapofika usiku.

Wamesema pia changamoto ya upatikanaji wa maji imepelekea kushindwa kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo na kuiomba Serikali kuingilia kati suala hilo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Fulwe, Saidi Katembo, hali hiyo imetokana na uharibifu wa Mabomba ya maji unaosababishwa na baadhi ya wananchi wasio waaminifu wanaoingilia miundombinu ya maji na kujiunganishia kinyume cha sheria