Ijumaa , 12th Sep , 2014

Msanii wa muziki mwenye mafanikio makubwa kutoka nchini Kenya, Jaguar amewataka mashabiki wake kuchukua hatua za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi, kwa kupima afya zao ili kujua hali zao.

msanii wa nchini Kenya Jaguar

Jaguar ambaye kwa sasa anafanya vizuri na rekodi yake inayokwenda kwa jina One Centimetre, binafsi ameonyesha mfano kwa kuanza kupima afya yake na kuweka majibu yake hadharani kupitia picha aliyoweka mtandaoni.

Kitendo cha msanii huyu kimetafsiriwa kwa namna tofauti huku asilimia kubwa ikimchukulia kama shujaa anayeiwazia mema jamii na maelfu ya mashabiki ambao wanamfahamu na kumfuatilia.