Jumamosi , 24th Aug , 2019

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri  Tanzania (KKKT), limemteua kwa mara nyingine tena Dkt. Fredrick Shoo, kuongoza tena kanisa hilo kwa kipindi cha miaka minne.

Askofu Dkt. Fredrick Shoo

Dkt. Shoo amechaguliwa usiku wa kuamkia Agosti 24, katika uchaguzi ambao alikuwa akichuana na maaskofu wengine takribani wanne waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Askofu Shoo alianza kuliongoza kanisa la KKKT tangu mwaka 2015, akiachiwa nafasi hiyo na aliyekuwa Askofu kwa kipindi hicho Dkt. Alex Malasusa.

Aliokuwa akichuana nao ni Dr. Steven Munga, Dr. Abednego Keshomshahara, Blaston Gavile na Dr. Alex Malasusa. Kati yao Dkt. Shoo amepata kura 144 na Dr. Keshomshahara amepata 74.