Jumamosi , 29th Jun , 2019

Bingwa wa dunia wa uzito wa juu, Andy Ruiz Jr, amemtambia Anthony Joshua kwa kusema sio bondia mzuri akiwa ulingoni na hata wakirudia mechi atamchapa tena.

Andy Ruiz Jr

Kibonge mwepesi huyo amesema hayo kwenye mkutano wa waandishi wa habari, baada ya kuwa na tetesi kuwa wawili hao wanataka kuzichapa kwa mara nyingine.

"Nishajua makosa yake, naweza kufanya kitu bora zaidi, kitu pekee anachoweza yeye ni kukimbiakimbia uwanjani, sio mzuri akiwa ulingoni tukirudia itakuwa vilevile".

Andy Ruiz Jr, amepata umaarufu mkubwa sana baada ya kumchapa bondia Anthony Joshua katika raundi ya saba katika mchezo uliopigwa Juni 1.

Hata hivyo promota wa bondia Anthony Joshua, amesema wawili hao wanaweza kuzichapa tena Novemba 16 au Decemba 14.