Rapa Nay wa Mitego
Nay ambaye amewahi kupanda katika majukwaa ya siasa 2015 kunadi wagombea wa UKAWA amesema kwamba ndoto zake ni kuwa Rais wa Tanzania mabaye hatakuwa na siasa nyingi zaidi ya kunyoosha mambo kama jinsi sasa hivi anavyonyoosha kwenye kazi za sanaa.
Akizungumza na www.eatv.tv, Nay amesema kwamba vishawishi vingi anavipata kutoka kwa wananchi na watu wengine wakimtaka aweze kugombea udiwani au ubunge lakini haoni kama nafasi hizo zinamstahili.
"Mimi nilishasema ninandoto za kuwa Rais wa nchi hii lakini sitakuwa Rais mwanasiasa. Nitahakikisha hakuna maneno maneno mengi zaidi ya kunyoosha kama ambavyo mambo yangu mengine nimekuwa nikinyoosha. Watu wanazungumza sana lakini niwaambie tu nashawishiwa sana na wananchi na baadhi ya viongozi wakiniomba nigombee lakini nimewaambia siwezi. Muziki ninaoufanya ni zaidi ya ubunge kwa sababu unawasaidia wananchi kuliko hao wanasiasa" Nay wa Mitego.
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuhusu msanii huyo anayesumbua na ngoma ya 'Mbele kwa mbele' kugombea jimbo la Ubungo ingawa haijawekwa wazi ni kwa chama gani cha siasa.