Jumatatu , 11th Aug , 2014

Baraza la Taifa la biashara TNBC limeyashauri mabaraza ya baishara ya mikoa ya nyanda za juu kusini kuanzisha vituo vitakavyotoa huduma za pamoja ili kukuza uwekezaji katika maeneo yao.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara nchini Tanzania (TNBC), Raymond Mbilinyi.

Akizungumza jijini Mbeya katibu mtendaji wa TNBC, Raymond Mbilinyi amesema serikali za mitaa zijenge mazingira wezeshaji na zisiwe vikwazo kwa uwekezaji ili kuharakisha maendeleo nchini.

Kwa upande wake Waziri wa nchi,Ofic ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji DK. Marry Nagu amesema kuna wawekezaji wengi wa ndani ambao wamefanya uwekezaji mkubwa katika mikoa ya kusini wanaostahili kupata hadhi ya uwekezaji mahiri lakini hawajapata nafasi hiyo.

Wakati huo huo, waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Injinia Christopher Chiza amezitakabodi za mazao nchini kutatua kero mbalimbali zinzowakabili wakulima ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha kwa wingi ili kufikia mahitaji ya soko la ndani na nje.

Chiza ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa wa wadau wa korosho Tanzania uliofanyika mkoani mtwara hivi karibuni na kuongeza kuwa bodi hizo za halamshauri zimekua na mianya ya wizi wa mifuko ya pembejeo kitu ambachop kinawaumiza wakulima.

Waziri Chiza amesema sababi za mianya hiyo ni wakulima kutoshirikishwa katika uamuzi kama kukokotoa hesabu za uendeshaji zinazohusu ununuzi,gharama za matumizi na malipo ya majaliwa ambayo ni kiini cha mafanikio kwa mkulima.