Alhamisi , 7th Aug , 2014

Rapa Chantelle kutoka nchini Kenya, anatarajia kuwa mama hivi karibuni baada ya kuonekana hadharani akiwa na ujauzito ambao bado haujafahamika una muda gani mpaka sasa.

msanii wa kike nchini Kenya Chantelle

Ujauzito huu wa Chantelle ambaye ni mwenzi wa mtayarishaji muziki J Blessing, umekuwa ni jambo la furaha kwa wawili hawa, huku Chantelle akijivunia kubadilishwa sana utaratibu wa maisha yake hasa baada ya kukutana na mwenzi wake huyu.

Chantelle amejijengea umaarufu na jina kubwa hasa kupitia rekodi iliyofanya vizuri sana ya Toklezea ambayo aliifanya na rapa Abbas Kubaff.