Jumamosi , 3rd Nov , 2018

Waziri wa Mali Asili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, ameweka wazi juu ya mpango wa kuwarudisha kwao watalii watakaoingia nchini, ambao watabainika kuwa wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Kigwangalla ameweka wazi msimamo huo kupitia ukurasa wake wa Twitter alipokuwa akijibizana na wafuasi wake ambao walikuwa wakijaribu kumuonya kuhusu kuingilia kati suala la 'ushoga' kuwa litaathiri utalii wa nchi.

Waziri Kigwangalla amesema kwamba watu hao watarudishwa kwao wakiwa uwanja wa ndege mara tu baada ya kutua.

Suala hili la kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja mkoani Dar es salaam, lipo chini ya ofisi ya mkuu wa mkoa Mh. Paul Makonda ambapo ameteua kamati maalum ya kushughulikia.