Alhamisi , 31st Jul , 2014

Rapa mkali wa nchini Kenya, Octopizzo amesema kuwa, imefika wakati wa mashabiki kwa kuanzia huko nchini Kenya, kuanza kukubali jitihada za wasanii wao katika kazi, na kuwaunga mkono kwa kununua kazi zao halisi.

msanii wa Kenya Octopizzo

Octopizzo amesema kuwa, mashabiki hususan nchini Kenya, wamekuwa na tabia ya kupenda vitu vya rahisi, na wamekuwa wakitumia pesa zao kununua kazi za wasanii ambazo zinatengenezwa kiholela mitaani bila wasanii husika kufaidika nazo.

Octopizzo amewataka mashabiki hawa kuzigeukia kazi halisi za wasanii hawa kama njia pia ya kuwainua na kutangaza zaidi kazi zao, hatua ambayo itainua sanaa nchini humo.