mashindano ya kucheza muziki Dance 100% 2014
Mashindano haya makubwa yamefikia hatua ya usaiili wa mwisho utakaofanyika Temeke jijini Dar es Salaam, katika viwanja vya TCC Chang'ombe Jumapili tarehe 3 mwezi Agosti.
Mpaka sasa makundi 10 tayari yamekwisha patikana ambapo yanaingia moja kwa moja hatua ya robo fainali ya mashindano haya makubwa nchini Tanzania.
Mchongo mzima kuhusiana na kile kilichofanyika Oysterbay na kufanikisha kupatikana kwa makundi matano, utaruka hewani kupitia show kali ya Dance100% ambayo itakujia kesho Jumatano, kuanzia saa moja kamili jioni hapa hapa EATV.