Jumatatu , 5th Feb , 2018

Kituo cha utangazaji East Africa Tv kimegeukia jamii ya wanawake nchini kwa kuanzisha kipindi kipya kitakachokwenda kwa jina la 'DADAZ' chenye lengo la kujadili mambo mbalimbali yanayotokea kwenye jamii katika mtazamo wa kike.

Kwa mujibu wa mtayarishaji wa kipindi hicho Sauda Wanguvu amesema kwamba 'DADAZ' ni platform ambayo ambayo itawagusa wanawake wenye kuanzia umri wa miaka 18-35 katika nyanja za kijamii, kisiasa na mengineyo mengi yanayotokea kwenye jamii inayowazunguka wanawake.

Aidha ameeleza kuwa lengo la kipindi hicho ni kuhabarisha na kuburudisha kwa njia tofauti tofauti kupitia mgawanyo wa vipengele vinne vilivyopo kwenye kipindi ambayo ni Soga, Mtu Kati, Madini na Chekecha.

Amefafanua kuwa ndani ya kipengelele cha Soga; mtazamaji atashuhudia majadiliano ya vitu ambavyo vina-trend kila siku katika jamii kama masuala ya elimu, siasa na mengineyo mengi, huku kipengele cha Mtu Kati chenyewe kikitoa fursa ya mahojiano na watu mbali mbali kupitia mada husika, taaluma na ufahamu wa jambo, na kumalizia kuwa  kipengele cha Chekecha chenyewe kitakuwa kikihusha burudani zote kwa ujumla.

Kipindi hicho cha DADAZ chenye muda wa saa 1 hewani  kitaongozwa na watangazaji watatu ambao ni Bhoke Egina, Dellaida Balyagati na Scola Kisanga