Jumapili , 29th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imeonya kuwafukuza kazi watumishi wa umma watakaohusika katika uidhinishaji wa malipo hewa.

Naibu waziri wa fedha na uchumi Mwigulu Nchemba.

Naibu waziri wa fedha na uchumi Mwigulu Lameck Nchemba amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi wa hoja za wabunge wakati wakichangia muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2014.

Katika kuhakikisha utekelezwaji wa agizo lake, naibu waziri Nchemba ameitaka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuweka mazingira yatakayoruhusu watumishi wa aina hiyo kufukuzwa kazi.