
Prof. Anangisye ameteuliwa katika nafasi hiyo kuitumikia kwa miaka mitano kuanzia leo Desemba 5, 2017. Makamu mkuu huyo mpya wa chuo anachukua nafasi ya Profesa Rwekaza S. Mkandala ambaye anamaliza muda wake.
Mkuu huyo wa chuo Dkt. Kikwete amefanya uteuzi huo baada ya kushauriana na bodi ya chuo kwenye kikao kilichofanyika Novemba 30 na baadae kumjulisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Kabla ya uteuzi wa leo Prof. Anangisye alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Elimu Dar es salaam (DUCE). Pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambaye aliteuliwa na Rais Mgaufuli.