Ijumaa , 28th Feb , 2014

Mwanadada Alicious Theluji, msanii kutoka Dr Congo ambaye makazi yake kwa sasa ni huko Nairobi nchini Kenya, amesema amefurahishwa kidogo kuona kuwa amani inarejea huko Mashariki mwa Congo ambapo alikuwepo kwa siku kadhaa hivi karibuni kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la Amani.

Alicious amesema kuwa, katika kipindi cha nyuma ilikuwa ni vigumu kukaa katika maeneo hayo kwa muda bila kusikia milio ya risasi, kitu ambacho sasa hakuna tena ikiwa ni dalili nzuri ya
utulivu na amani kwa maeneo hayo.

Alicious pamoja na ndugu zake, ni moja kati ya familia nyingi ambazo ziliamua kuhama huko nchini Congo kwa ajili ya kuepusha hatari ya kupoteza maisha kutokana na machafuko ya amani ambayo yamekuwa yakiendelea nchini humo kwa miaka mingi sasa.