
Mkuu wa vipindi vya East Africa Radio Nasser Kingu (Kushoto) na mtangazaji wa EATV, Suzy, wakiendesha droo ya tatu kupanga ratiba ya michuano ya Sprite BBall Kings iliyofanyika usiku wa kuamkia leo.
Michuano hiyo itakayoshirikisha timu nane (8) ambazo ziliweza kufuzu hatua ya awali na kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi Julai Mosi katika uwanja ambao utatangazwa hapo baadae.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Kocha wa timu ya vijana (U-16), Bahati Mgunda amewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika mashindano hayo ili waweze kuonesha vipaji vyao walivyokuwa navyo pamoja na kuwapa fursa watazamaji kuweza kuona mashindano mazuri.
"Nia kubwa ya mashindano haya nikuinua vipaji, kuinua mchezo huu wa kikapu kwa hiyo kwa 'support' mnayoipata mimi naomba muitumie vilivyo, kwa kuwa mashindano haya yamerudishwa mtaani zaidi na siyo ya kwenda kuchezea ughaibuni. Kama ni vita basi hii ni vita nzuri kwani pale ukishamjua mshindani wako ni nani unaweza kujipanga vizuri nawasihi wachezaji mjipange vizuri baada ya kutoka hapa ili muweze kufanya vizuri zaidi katika mechi za robo fainali" alisema Kabinda
Wawakilishi wa timu mbalimbali waliohudhuria kushuhudia droo ya wazi ya tatu michuano ya Sprite BBall Kings
MATOKEO YA DROO
Hii ndiyo ratiba kamili ya michuano ya Sprite BBall Kings itakayoanza kutikisa siku ya Jumamosi ya Julai Mosi kwa mechi nne katika hatua ya robo fainali.