
Hayo Sheddy amefunguka mbele ya kamera za EATV na kudai kwamba muziki wa sasa umevamiwa na watu wengi wasiokuwa na taaluma pamoja na viwango vya kutengeneza muziki, hali inayofanya muziki wa Tanzania kushuka kila siku na hata ile hatua iliyokuwa inawakaribia wa Nigeria imerudi nyuma kwa kiasi kikubwa
Aidha Sheddy ameongeza kwamba serikali inapaswa kuweka viwango na sheria ya kudhibiti maprodyuza na kugawa hatimiliki kwa watu wachache wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo ili kuweza kushindana na masoko ya nchi mbali mbali.
"Ma - prodyuza feki ni wengi sana wale waliopo real ni wachache sana. Zamani kina P. Funk walikuwa wanatengeneza nyimbo zinadumu muda mrefu na ni kali lakini za sasa hivi imebidi ma - director wa video wawe wabunifu kutengeneza video kali ili wimbo uonekane ni mzuri"- Sheddy alifunguka
Pamoja na hayo Sheddy amefunguka na kusema serikali inapaswa pia kusimama na kuangalia maslahi ya watayarishaji wa muziki kwani wamekuwa wakiwatajirisha wasanii huku wao wakibaki kwenye maisha yale yale.
"Upande wa maslahi inabidi serikali ijipange ituwekee maslahi mazuri kwani mtayarishaji wa muziki kama anahitaji maisha mazuri itambidi awe anakazi nyingine na siyo kutegemea production tuu. Unaweza ukawa na hit kibao redioni lakini maisha yako yakawa ya tabu sana"- Sheddy aliongeza.